JESHI LA POLISI HARAKISHENI UCHUNGUZI WA MWANAFUNZI -TAMWA ZNZ

 NA MWANDISHI WETU,

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ) kinaliomba, Jeshi la Polisi kuharakisha uchunguzi wa kifo cha mtoto Raiyan Hemed Amour (15),mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika skuli ya Sekondari Kizimbani.

Wilaya ya  Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ambaye mwili wake ulidaiwa kukutwa katika kichaka huku kiganja cha mkono wake wa kulia kikiwa kimekatwa na kitu chenye ncha kali.

Kwa muijibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa tarehe 5/10/2026, mwili wa Raiyan, ulionekana katika kichaka akiwa amefariki dunia baada ya kuondoka nyumbani kwao, Kijiji cha Kwale Mpona siku ya Ijumaa Oktoba 2, 2026 majira ya saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya kwenda skuli.

TAMWA ZNZ,  inaomba uchunguzi wa kina na haraka ufanyike ili kubaini mazingira ya kutoweka na hatimae kifo cha Raiyan ili mtu au watu waliohusika na ukatili huo, wanabainishwa na kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria. Hatua hiyo ni muhimu katika kujenga imani ya wananchi katika mifumo ya haki na ulinzi wa watoto.

 Aidha, hatua madhubuti dhidi ya wahusika zitatoa ujumbe wa wazi kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya watoto havitavumiliwa katika jamii.

Juhudi kubwa zimekuwa zikifanywa na Serikali pamoja na mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kuimarisha haki za wanawake na watoto, hususan katika kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanapata fursa sawa za elimu, ulinzi na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii, baada ya kuachwa nyuma katika nyanja mbalimbali za maendeleo kwa muda mrefu.

 Juhudi hizi zimewezesha kupatikana kwa mafanikio makubwa, na hivyo zinapaswa kuendelezwa na kuimarishwa zaidi ili kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayepoteza maisha, kunyimwa fursa au kuishi katika mazingira ya hofu na ukosefu wa usalama.

TAMWA ZNZ imekuwa ikishauri Jeshi la Polisi pamoja na taasisi nyengine za haki kwa muda mrefu kutangaza hatua ambazo zinafikiwa katika kushughulikia kesi kama hizi za ukatili kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazolinda taarifa nyeti za waathirika na watoto ambapo tokea mwishoni mwa mwaka 2016 imeshuhudia jumla ya matukio 34 ya mauaji wanawake (27) na watoto (7).

 Jamii haijajuilishwa ipasavyo mwenendo wa kesi hizo na hukumu zake jambo ambalo linahitaji kubadilika ili kuongeza uwazi, uwajibikaji na imani ya wananchi katika mifumo ya haki.

KUIMARISHA USALAMA WA WATOTO NJIANI NA MAENEO YA SKULI

Sambamba na uchunguzi wa tukio hili, TAMWA-ZNZ inaiomba Serikali, kupitia mamlaka husika, kuhakikisha kuwa mazingira yanayowazunguka watoto yanakuwa salama, hususan wakati wanapokwenda na kurudi skuli.

Serikali na mamlaka za maeneo zinapaswa kuchukua hatua za kupunguza au kuondoa vichaka na maeneo mengine hatarishi yaliyo karibu na makazi ya watu na njia zinazotumiwa na watoto ambazo zitasaidia kupunguza hofu na hatari zinazoweza kuwakabili watoto, hususan wasichana, wanapokuwa njiani.

ZANZIBAR NA MALENGO ENDELEVU YA MAENDELEO

Zanzibar, kama sehemu ya dunia, inatekeleza Malengo Endelevu ya Maendeleo (Sustainable Development Goals – SDGs) yanayolenga kufikiwa ifikapo mwaka 2030.

TAMWA-ZNZ inasisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Lengo la 5 la SDGs, linalolenga kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana kuishi bila ubaguzi na ukatili.

Aidha, tukio hili linahusiana pia na Lengo la 16, linalohimiza kujenga jamii zenye amani, upatikanaji wa haki kwa wote na taasisi inazowajibika na zinazofanya kazi kwa ufanisi.

Utekelezaji wa malengo haya unapaswa kuonekana kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa dhidi ya ukatili, napata mazingira salama nawanapofanyiwa ukatili, mifumo ya haki inachukua hatua kwa haraka na kwa ufanisi.

MSAADA WA KISAIKOLOJIA KWA WATOTO

Aidha, TAMWA-ZNZ inaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, kutoa huduma na msaada wa kisaikolojia kwa watoto wanaoishi katika Kijijicha Kwale na maeneo yanayozunguka tukio hili, hususan watoto wanaoweza kuwa  wameathirika kwa hofu, msongo wa mawazo au mshtuko kutokana na tukio hilo.

Hatua hiyo ni muhimu ili kuwasaidia watoto kukabiliana na athari inazoweza kujitokeza kutokana na tukio hili na kuhakikisha wanaendelea na shughuli zao za kila siku bila ya kubeba madhara ya muda mrefu ya kisaikolojia.

TAMWA ZNZ inanaendelea kutoa pole kwa familia ya marehemu ndugu, jamaa, walimu, wanafunzi wenzake Raiyan Hemed Amour kwa msiba huu mzito.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Raiyan mahali pema peponi, na awape wafiwa subira, nguvu na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

 UCHUNGUZI WA KIFO CHA MTOTO RAIYAN HEMED AMOUR.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ) kinaliomba, Jeshi la Polisi kuharakisha uchunguzi wa kifo cha mtoto Raiyan Hemed Amour (15),mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika skuli ya Sekondari Kizimbani, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ambaye mwili wake ulidaiwa kukutwa katika kichaka huku kiganja cha mkono wake wa kulia kikiwa kimekatwa na kitu chenye ncha kali.

Kwa muijibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa tarehe 5/10/2026, mwili wa Raiyan, ulionekana katika kichaka akiwa amefariki dunia baada ya kuondoka nyumbani kwao, Kijiji cha Kwale Mpona siku ya Ijumaa Oktoba 2, 2026 majira ya saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya kwenda skuli.

TAMWA ZNZ inaomba uchunguzi wa kina na haraka ufanyike ili kubaini mazingira ya kutoweka na hatimae kifo cha Raiyan ili mtu au watu waliohusika na ukatili huo, wanabainishwa na kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria. Hatua hiyo ni muhimu katika kujenga imani ya wananchi katika mifumo ya haki na ulinzi wa watoto.

 Aidha, hatua madhubuti dhidi ya wahusika zitatoa ujumbe wa wazi kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya watoto havitavumiliwa katika jamii.

Juhudi kubwa zimekuwa zikifanywa na Serikali pamoja na mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kuimarisha haki za wanawake na watoto, hususan katika kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanapata fursa sawa za elimu, ulinzi na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii, baada ya kuachwa nyuma katika nyanja mbalimbali za maendeleo kwa muda mrefu.

 Juhudi hizi zimewezesha kupatikana kwa mafanikio makubwa, na hivyo zinapaswa kuendelezwa na kuimarishwa zaidi ili kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayepoteza maisha, kunyimwa fursa au kuishi katika mazingira ya hofu na ukosefu wa usalama.

TAMWA ZNZ imekuwa ikishauri Jeshi la Polisi pamoja na taasisi nyengine za haki kwa muda mrefu kutangaza hatua ambazo zinafikiwa katika kushughulikia kesi kama hizi za ukatili kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazolinda taarifa nyeti za waathirika na watoto ambapo tokea mwishoni mwa mwaka 2016 imeshuhudia jumla ya matukio 34 ya mauaji wanawake (27) na watoto (7).

 Jamii haijajuilishwa ipasavyo mwenendo wa kesi hizo na hukumu zake jambo ambalo linahitaji kubadilika ili kuongeza uwazi, uwajibikaji na imani ya wananchi katika mifumo ya haki.

KUIMARISHA USALAMA WA WATOTO NJIANI NA MAENEO YA SKULI

Sambamba na uchunguzi wa tukio hili, TAMWA-ZNZ inaiomba Serikali, kupitia mamlaka husika, kuhakikisha kuwa mazingira yanayowazunguka watoto yanakuwa salama, hususan wakati wanapokwenda na kurudi skuli.

Serikali na mamlaka za maeneo zinapaswa kuchukua hatua za kupunguza au kuondoa vichaka na maeneo mengine hatarishi yaliyo karibu na makazi ya watu na njia zinazotumiwa na watoto ambazo zitasaidia kupunguza hofu na hatari zinazoweza kuwakabili watoto, hususan wasichana, wanapokuwa njiani.

ZANZIBAR NA MALENGO ENDELEVU YA MAENDELEO

Zanzibar, kama sehemu ya dunia, inatekeleza Malengo Endelevu ya Maendeleo (Sustainable Development Goals – SDGs) yanayolenga kufikiwa ifikapo mwaka 2030.

TAMWA-ZNZ inasisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Lengo la 5 la SDGs, linalolenga kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana kuishi bila ubaguzi na ukatili.

Aidha, tukio hili linahusiana pia na Lengo la 16, linalohimiza kujenga jamii zenye amani, upatikanaji wa haki kwa wote na taasisi inazowajibika na zinazofanya kazi kwa ufanisi.

Utekelezaji wa malengo haya unapaswa kuonekana kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa dhidi ya ukatili, napata mazingira salama nawanapofanyiwa ukatili, mifumo ya haki inachukua hatua kwa haraka na kwa ufanisi.

MSAADA WA KISAIKOLOJIA KWA WATOTO

Aidha, TAMWA-ZNZ inaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, kutoa huduma na msaada wa kisaikolojia kwa watoto wanaoishi katika Kijijicha Kwale na maeneo yanayozunguka tukio hili, hususan watoto wanaoweza kuwa  wameathirika kwa hofu, msongo wa mawazo au mshtuko kutokana na tukio hilo.

Hatua hiyo ni muhimu ili kuwasaidia watoto kukabiliana na athari inazoweza kujitokeza kutokana na tukio hili na kuhakikisha wanaendelea na shughuli zao za kila siku bila ya kubeba madhara ya muda mrefu ya kisaikolojia.

TAMWA ZNZ inanaendelea kutoa pole kwa familia ya marehemu ndugu, jamaa, walimu, wanafunzi wenzake Raiyan Hemed Amour kwa msiba huu mzito.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Raiyan mahali pema peponi, na awape wafiwa subira, nguvu na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

No comments

Powered by Blogger.