TUNATAKA WANDISHI WA HABARI MJILINDE -UTPC
NA MARYAM NASSOR
WANDISHI wa Habari wametakiwa kuzingatia usalama wao
kwanza wakati wakitimiza majukumu yao kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu 2025.
Akitoa
mafunzo kwa wandishi wa Habari 15 kutoka klabu za wandishi wa Habari huko mjini
Morogoro Mkufunzi katika mafunzo hayo Neville
Meena .
Amesema
, mwandishi wa Habari usalama wake ni muhimu , tishio lolote likimpata mwandishi litasababisha kazi anayotaka
kuifanya asiifanye ipasavyo.
“ Kwa hiyo tunawataka wandishi wa Habari kuwa salama
kwa namna moja au nyengine na
usalama wenu ndio utasababisha ujumbe munaotaka kuufikisha kwa jamii
kufika kwa urahisi.” amesema Meena.
Amesema
kuwa, wanahitaji mwandishi wa Habari asipate shida yoyote kama kupigwa , kunyang’anywa
vifaa , kuumizwa na hata tatizo la kutekwa na kuumia .
“ Kuna
mwandishi mwenzetu Azori Mziwanda alipotea siku nyingi zilizopita na hatujui alipo , hivyo tunataka kesi kama hizo zisijirudie tena ” amesema Meena.
Aidha amesema kuwa, usalama wa mwandishi wa Habari
unaanza na yeye mwenyewe , kujitambua yeye ni nani anafanya kazi nan ani na
mambo mengine mengi ili achukuwe tahadhari mapema na asijikute ameingia katika
matatizo yatakayo mfanya asifanye kazi au kutekeleza wajibu wake.
Nae, Lulu George Mtaalamu wa Maswala ya Saikolojia na
mkufunzi katika mafunzo hayo ,amesema
kuwa ni kweli wandishi wa Habari wanakutana na matatizo mbali mbali
yanayohusu maswala ya kisaikolojia na wahanga wakuu kutokana na kazi
wanazozifanya.
Amesema
kuwa, wandishi ndio wanaoripoti majanga
mbali mbali yakiwemo ajali kwa afya ya akili inakuwa ni tatizo lakini kutokana
na hali zao wanakosa msaada wa kitaalamu kwa sababu unahitaji gharama na hakuna
mtu wa kuwasemea wala kuwapigania.
“ Katika mafunzo haya tumewafundisha ustawi wa afya zao ikiwemo kimwili na akili ili waweze kujilinda na kutekeleza majukumu yao” amesema Lulu.
Victor Maleko Afisa Mafunzo kutoka UTPC amesema mafunzo hayo yamelenga wandishi wa Habari ambao wataenda kutoa mafunzo kwa wandishi wengine kuhusu usalama wa kimtandao, kisaikolojia na usalama wa kimwili .
Amesema kuwa, kitu kilichomfurahisha katika mafunzo hayo ni kuona kuwa Ushahidi wa matukio ambayo yalishawahi kuwapata wandishi wengine wa Habari na kuweza kuyatatua .
“ Nimefurahi
kwa kuweza kupata timu nzuri ya wandishi wa Habari hawa waliyopatiwa
mafunzo naamini wakienda huko katika
mikoa waliyotoka wataweza kuifikisha elimu na ujuzi waliyoupata hapa”
Aidha ameendelea kuwasihi wandishi wa Habari kuendelea kubaki katika mazingira salama na rafiki wakati wakitimiza wajibu wao, na kuwaasa kuwa usalama wa mwandishi wa Habari unaanza na yeye mwenyewe.

Nao,baadhi ya Wandishi wa Habari waliyopata mafunzo hayo wameahidi kuifikisha elimu hiyo
kwa wandishi wenzao katika klabu zao na wandishi wengine wenye uhitaji.
Aidha
wameishukuru UTPC kwa kuwachaguwa wao
kuwa sehemu ya wakunzi ( TOT) ambao wataenda kuwafundisha wenzao.
Mafunzo hayo
ya siku tatu yamewashirikisha wandishi wa Habari 15 kutoka katika klabu za wandishi wa Habari mbali
mbali Tanzania, yameandaliwa na Umoja
wa Klabu za Wandishi wa Habari Tanzania (UTPC).



Post a Comment