RUSHWA MUHALI NI SUALA LILILOPITWA NA WAKATI - TAMWA ZNZ
NA MARYAM NASSOR
MKURUGENZI
wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA ZNZ)Nairat Abdulla Ali amesema
rushwa muhali ni suala lililopitwa na
wakati na kuitaka jamii kushirikiana pamoja ili kuwanusuru manusura wa
vitendo hivyo.
Akizungumza
katika ukumbi wa chama hicho uliopo Tunguu, Unguja, wakati wa kikao na wadau wa
mtandao wa kupinga udhalilishaji Zanzibar, amesema kuwa vitendo vya rushwa ya muhali vinaathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa
wanawake na wasichana, hususan katika maeneo ya vijijinii.
Ameeleza
kuwa, licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali na mashirika yasiyo
ya kiserikali, bado baadhi ya wahusika wanatumia nafasi zao vibaya kwa kuomba
au kushinikiza rushwa muhali, jambo
linalodumaza haki na usawa katika jamii.
Akibainisha
kuwa“ ukimya unaochangiwa na hofu na unyanyapaa umekuwa kikwazo kikubwa katika
mapambano dhidi ya vitendo hivyo” amesema .
Aidha,
amesisitiza umuhimu wa elimu kwa umma ili kuongeza uelewa kuhusu haki za msingi
na madhara yanayowapata wanawake na wasichana .
Kwa upande
wake Manager wa kitengo cha mawasiliano
kutoka TAMWA ZNZ Bi Sophie Ngalapy.
amesisitiza umuhimu wa kuheshimiana
mkubwa kumuheshimu mdogo na mdogo kumuheshimu
mkubwa ili kujiepusha na vitendo vya udhalilishaji .
Amesema kuwa, elimu ni muhimu sana katika kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji katika jamii ili kumaliza matendo haya nchini.
Kwa upande
wake, mmoja wa wasaidizi wa sheria wilaya ya kaskazini ‘A’ Unguja Asya Fadhil Makame amesema kuwa kuna haja ya
kuimarisha mifumo ya kuripoti matukio ya udhalilishaji ili manusura waweze
kupata msaada wa haraka na haki stahiki bila kuogopa.
Ameongeza
kuwa, ushirikiano kati ya taasisi za
serikali, asasi za kiraia na jamii kwa ujumla ni muhimu katika kuhakikisha
vitendo vya rushwa ya muhali vinatokomezwa
kabisa.
Naye, mwakilishi wa Un Women Tanzania kwa upande wa Zanzibar Jesca Msafiri amesema, vitendo vya udhalilishaji vinahitaji ushirikiano wa Pamoja kati ya Serikali na wadau mbali mbali.
Amesema, takwimu za vitendo vya udhalilishaji Tanzania vinaonesha kwa kila wanawake 40 wanne wamefanyiwa vitendo hivyo, na kila wanaume 10 mmoja amefanyiwa vitendo
vya udhalilishaji.
“ Takwimu
hizi ni kwa wale wanaoripoti
matendo haya, lakini baadhi ya
wanajamii bado hawaripoti vitendo vya udhalilishaji kutokana na kukosa elimu na muhali” amesema.
Nao , washiriki wa kikao hicho wamependekeza kuanzishwa kwa kampeni endelevu
zitakazolenga kubadili mitazamo hasi ya jamii pamoja na kuwajengea uwezo
wanawake na wasichana kujitambua na kujilinda dhidi ya vitendo vya
udhalilishaji.



Post a Comment